SAMO LAY AFUNGUKA MAZITO KUHUSU BOB JUNIOR

Samo lay, mkali wa Koroboi aliyetokea Rubi Band, amefunguka kuhusu maisha yake na Bob Junior.




Akiongea na Hotmixmziray, amebainisha kuwa amewahi kuishi kwa Rais wa Sharobaro, Bob Junior, lakini kwa maneno tu, bila kutoka kimuziki, tofauti na alivyoahidiwa, huku akiishia kurekodi ngoma tatu, tofauti na alivyotegemea.

“Nimeishi kwa Bob Junior kwa maneno, nimerekodi nyimbo kama tatu, mpaka sasa, lakni sijazifanyia video. Kila nilipokuwa nikimuomba Bob Junior kuwa nimepata mtu, nataka nifanye nae project, alikuwa anagoma kunipa hizo ngoma” amesema samo Lay.

Mkataba niliokuwa nao pale ni wa maneno tu, hatukuwahi kusainishana chochote. Nilipoona hivyo nikaamua kutoka SharoBaro na mpaka sasa, hajanipa ngoma zang. Bado zipo SharoBaro alizungumza Samo Lay.

Comments