Muimbaji mkongwe wa muziki Q Chief amesema show yake ya ‘Miaka 15 ya Q Chief’ katika muziki inayotarajia kufanyika April 30 katika ukumbi wa Next Door, Masaki, jijini Dar es salaam itakuwa ni show ambayo itabeba mambo mengi yakumtoa machozi kutokana na changamoto alizozipitia katika maisha ya muziki.
Q Chief amesema atatumia show hiyo kumtambulisha mama watoto wake kama miongoni mwa watu waliompigania katika nyakati zote.
“Show hii itakuwa ni burudani lakini pia naweza kulia kwa machungu, kwa sababu nimepitia mambo mengi sana katika safari ya muziki wangu,” alisema Q Chief. “Namshukuru mpenzi wangu, mwanangu mpendwa, wazazi wangu pamoja na wadau wengine ambao bado wanaendelea kunipigania kuhakikisha nafika sehemu fulani,”
Alisema katika show hiyo atasindikizwa na wasanii mbalimbali ambao amekuwa akishirikiana nao katika muziki kwa kipindi hicho chote.
Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii ambao waliingia katika lindi la kutumia dawa za kulevya lakini alifanikiwa kuacha.

Comments
Post a Comment