MUUAJI ALIVYOONEKA FACEBOOK AJIUA

Mahusiano na madeni kwenye mchezo wa kamari yalimsukuma Stevens kutekeleza mauaji
Mahusiano na madeni kwenye mchezo wa kamari yalimsukuma Stephens kutekeleza mauaji

Polisi nchini Marekani wamesema mtu ambaye alifanya mauaji kisha kutuma video ya mauaji hayo katika mtandao wa Facebook amejiua mwenyewe.
Wamesema Steve Stephens alijiua wakati maafisa wa polisi walipolikaribia Gari lake walipokuwa wakimkimbiza takribani kilomita 150 kutoka Cleveland, Ohio, eneo la mauaji yaliyofanyika jumapili.
Picha za video za babu akipigwa risasi zilisalia kwenye mitandao ya kijamii kwa saa mbili bila kuondolewa.
Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg, alieleza maskitiko yake kwa ndugu na akaahidi kuwa kampuni itafanya kila linalowezekana kuzuia jambo kama hilo kuwekwa tena mtandaoni.

Comments