Ugo Ehiogu alichezea timu ya taifa ya England mechi tano
Beki wa zamani wa timu ya taifa ya England na Aston Villa Ugo Ehiogu amefariki akiwa na umri wa miaka 44 baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo Alhamisi.
Ehiogu alipatwa na mshtuko wa moyo akiwa katika kituo cha mazoezi cha klabu ya Tottenham Hotspur.
Taarifa ya Spurs ilsiema Ehiogu alifariki mapema Ijumaa akiwa hospitalini.
Ehiogu, ambaye alikuwa mkufunzi wa timu ya Spurs ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23, alikuwa amechezea timu ya taifa ya England mechi nne na kufunga bao moja.
"Hatuwezi kueleza majonzi na huzuni tuliyo nayo katika klabu hii," mkuu wa ukufunzi na ustawi wa wachezaji Tottenham John McDermott amesema.
Ehiogu alichezea Atson Villa karibu mechi 200 kati ya 1991 na 2000 kisha akacheza miaka saba Middlesbrough.
Alishinda Kombe la Ligi akiwa na Villa mwaka 1994 na 1996 na pia akiwa na Boro mwaka 2004.
Beki huyo pia alichezea West Brom, Leeds, Rangers na Sheffield United, kabla ya kustaafu 2009.
Alianza kazi ya ukufunzi Tottenham mwaka 2014.
Ehiogu alikaa miaka tisa Aston Villa
Ehiogu alijiunga na Middlesbrough mwaka 2000 kwa £8m
Ehiogu alifungia England dhidi ya Uhispania mechi ya kirafiki 2001
Comments
Post a Comment