Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki
Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki 'alipuuzwa' na Marekani wakati wa ziara yake ya hivi karibuni mjini Washington kulingana na jarida la Foreign Policy FP.
Bwana Faki alikuwa amealikwa nchini humo na waziri wa maswala ya kigeni nchini humo Rex Tillerson wiki ya tarehe 17 mwezi Aprili lakini afisi ya Tillerson haikuthibitisha mkutano huo na ikawasiliana na Faki wakati alipokuwa akiondoka kuelekea mjini New York.Wizara ya maswala ya kigeni badala yake ilitaka bwana Faki kufanya mkutano na afisa wa ngazi za chini hatua iliomfanya Faki kufutilia mbali ziara yake yote ya Washington kulinga na FP.
Reuben Brigety , balozi wa zamani wa Marekani katika Umoja wa Afrika aliyehojiwa amesema kuwa huenda utawala wa rais Trump unafanya makosa makubwa ama pengine hauoni uhusiano kati yao na Afrika kuwa kitu muhimu.
''Huu ni ujinga, wakati ambapo bara la Afrika linaendelea kujua kuhusu chaguo lao kuhusu ushirikiano wao duniani''.
Ameongezea kuwa sio mara ya kwanza kwa utawala huo kupuuzilia mbali viongozi wa Afrika.
Mnamo mwezi Machi, rais wa Rwanda Paul Kagame alizuru Washington na hakuna mtu katika wizara ama hata Ikulu ya Whitehouse aliyekuatana naye, ripoti hiyo imesema.
Comments
Post a Comment