Waandamanaji Venezuela
Maelfu ya raia wa Venezuela wameandamana katika mji mkuu wa Caracas na katika miji mingine zaidi ya 20. Waandamanaji wanataka kufanyike uchaguzi wa Urais na kuachiliwa huru kwa wanasiasa wa upinzani.
Wafuasi wa Rais Nicolas Maduro pia wamekua wakiandamana katika mji mkuu wa Caracas, kama ishara ya kumuunga mkono kiongozi huyo.Licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta, Venezuela imeendelea kukumbwa na mfumuko mkubwa wa bei, visa vingi vya uhalifu na uhaba wa bidhaa muhimu.
Comments
Post a Comment