Joseph Kony kiongozi wa waasi wa LRA
Jeshi la Uganda limesema kwamba maafisa wake wa kijeshi wameanza kuondoka katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati ambapo wamekua wakikabiliana na waasi kutoka Uganda wa kundi la 'Lord's Resistance Army'-LRA.
Kundi la LRA linaloongozwa na Joseph Kony limelaumiwa kwa kutekeleza uhalifu wa kibinadamu dhidi ya raia wa Kaskazini mwa Uganda katika miaka ya 90 hadi 2000. Kony na wapiganaji wake walifurushwa Uganda na kukimbilia nchi jirani ya Sudan Kusini.
Baadaye walihamia katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati kufuatia shinikizo za kimataifa.
Jeshi la Uganda limesema LRA haina uwezo tena wa kuanzisha vita dhidi ya Uganda, baada ya nguvu zake kupungua
Comments
Post a Comment