LINAH SIKU ZA KUJIFUNGUA ZINAKARIBIA

Kuashiria siku zinakaribia, mama kijacho huyo wa bongo flava, Linah Sanga ametuonyesha muonekano wa kitanda cha mwanae.
Kitanda hicho cha mtoto kimepostiwa kupitia Instagram ya mwanamuziki huyo, huku kikiwa kimepambwa na midoli na mito.



Linah ambaye amekataa kutaja jinsia ya mtoto wake mtarajiwa ila tu kututajia herufi ya jina la mtoto wake kuwa ni “T” ameendelea kupost picha mbali mbali za ujauzito wake huku akiwa na furaha.
Hili sio jambo la kushangaza kwa kipindi hiki, kuona mastaa wakionyesha kufurahia hali zao za ujauzito na ujio wa watoto katika maisha yao.

Comments