Michezo ya Play off ya Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2016/2017 imeendelea tena leo April 26 kwa michezo minne kuchezwa, KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta walikuwa ugenini kucheza mchezo wao wa 5 wa play off wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya wenyeji wao AS Eupen.
KRC Genk waliingia uwanjani kucheza mchezo huo wakiwa wana rekodi ya kuwa timu pekee katika timu 12 zinazocheza game za play off kutofungwa mchezo hata mmoja wakiwa wameshinda michezo yote minne, leo KRC Genk wakiwa ugenini wamelazimishwa sare ya 1-1 na kuwafanya kupata sare ya kwanza
AS Eupen licha ya kuwa nyumbani walianza kufungwa goli dakika ya 20 Malinovsky akipachika goli la kwanza la Genk lakini AS Eupen walisawazisha goli hilo dakika ya 51, katika michezo ya play off KRC Genk na AS Eupen ndio timu pekee ambazo hazijapoteza mchezo katika timu 12 za Kundi A&B lakini AS Eupen wameshinda game moja pekee kati ya tano.
Comments
Post a Comment