JUMA NATURE ANASEMA HAWEZI KUGOMBANA NA CHEGE


Msanii mkongwe nchini Tanzania,Juma Nature maarufu kama "Kiroboto" amefunguka na kusema hajawahi na kugombana na msanii mwenzake Chege Chigunda kama watu wanavyofikiri kuwa mwanamke ndiyo amewafanya washindwe hata kusalimiana wawili hao.

Nature amebainisha hayo baada ya kuenea tetesi za kipindi kirefu zilikuwa zinawaaminisha watu kuwa mke aliyemuoa msanii huyo ndiye alikuwa mpenzi wa chege hapo awali mpaka kupelekea kuimba wimbo wenye maudhui ya kumuaga mpenzi huyo uliopewa jina la "Good bye"
"Mimi sijawahi kugombana na mwanangu, sasa mimi nigombane na damu itawezakana kweli?,hatuwezi kugombana, tutagombana stejini tu kwa sababu ya usanii lakini hatugombani kama hivyo unavyochukulia wewe" Alisema Juma Nature pindi alipokuwa anazungumza katika kipindi cha eNEWS ya EATV

Comments