Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ .
MWANADADA anayefanya vizuri kwenye Muziki wa Bongo Fleva na wimbo wake wa Usimwache, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amechekelea kufanya kolabo na mwanamuziki wa nje ya nchi huku akisema kwamba anaona ndoto zake zinaenda kutimia.
Akipiga stori na Risasi Vibes, Lulu Diva alisema anamshukuru Mungu kwani amefanya kolabo na mwanamuziki wa Zimbabwe, Jahprazy jambo ambalo limempa faraja na kuona mwanga wa ndoto zake za kutoka kimataifa zikitimia.
“Kwenye u-video queen nilikuwa napoteza sana muda kwa kweli, ndiyo maana sipendi kabisa kuitwa jina hilo kwani sasa hivi nimejikita moja kwa moja kwenye muziki na ndoto zangu za kutoka kimataifa naona zimeshaanza kutimia,“ alisema Luku Diva na kuongeza:
“Nimefurahi sana kufanya kolabo na huyo msanii wa Zimbabwe ambaye pia aliwahi kuimba na Diamond ambayo wimbo unatarajiwa kutoka hivi karibuni, hivyo mashabiki wangu wasubiri kutusikia
Comments
Post a Comment