DR KIGWANGALA AMPA PONGEZI DIAMOND

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamisi Kigwangalla, ameueleza umma kuwa hajawahi kuwa shabiki wa Mwanamuziki, Diamond Platnumz ila tangu aanze kumfuatilia amegundua kuwa ni mjasiriamali mzuri na kumwagia sifa nyingi.


Dkt Kigwangalla ameandika hayo, Jumatatu hii kupitia ukurasa wake wa Instagram akisema

Sikuwahi kuwa mshabiki wa msanii huyu kijana @diamondplatnumz, kama nilivyosema hapo nyuma kidogo, japokuwa nimekuwa nikifuatilia na ku-enjoy muziki wake; Ila toka nimeanza kumfuatilia nimegundua kuwa, this young man is not only a good entertainer, but also a talented entrepreneur and businessman. He does business in music, he does a business of entertainment. Sasa naona kupitia kipaji chake cha ujasiriamali, ameamua kuwa muwekezaji, an investor! This is incredible. Keep stepping up your game son, that’s the way to do it! Hakika wewe umetoka #NjeYaBox, na Mungu akuongoze ubaki huko huko juu, usishuke! I wish wasanii wenzako pia watoke nje ya box kifikra, wafanye biashara kwenye vipaji vyao, wageuze changamoto kuwa fursa, waache kulalamika, wapige kazi tu! #HapaKaziTu! Kwa sababu nyie watu mashuhuri mkigeuza crowds zenu kama chanzo cha solo la bidhaa zenu, kwa hakika mtafanikiwa sana! Changamoto kwenu wadogo zangu…#chibudangote #chibu #diamondplatnumz #MzeeWaField #Dr_Kigwangalla #HamisiKigwangalla #SiasaNiVitendo #supportingourown #MadeInTanzania #Tanzanian #ProudlyTanzanian Pongezi nyingi kwa team nzima nyuma ya Diamond @sallam_sk @babutale @mkubwafellatmk

Comments