Korea Kaskazini inaendelea kufanyia silaha majaribio licha ya kuwepo msukosuko
Rais wa China Xi Jinping ametaka kuwepo uvumilivu kutoka pande zote wakati wa mawasiliano ya simu na rais wa Marekani Donald Trump siku moja baada ya Korea kusema kuwa ilikuwa tayari kuzamisha meli ya kubeba ndege za vita ya Marekani.
Mawasiliano hayo ya simu ndiyo ya pili kati ya viongozi hao wawili tangu wakutane huko Florida mapema mwezi huu.Ni ishara ya hofu ya China kuwa msukosuko kati ya Marekani na Korea Kaskazini utasababisha mzozo.
Siku ya Jumapili vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vilisema kuwa jeshi la Korea Kaskazini lilikuwa tayari kuzamisha meli ya Marekani ya USS Carl Vinson, ambayo Marekani inasema itawasili katika rasi ya Korea siku chache zinazokuja.
Meli hiyo ilitumwa na Rais Trump huku onyo ikitolewa kuwa Marekani imepotza uvumilivu kwa mipango ya nuklia ya Korea Kaskazini.
USS Carl Vinson ikiwa bahari ya Hindi
Wakati wa mazungumzo hayo ya simu Bwana Xi alitaka pande zote kuwa wavumulivu na kuzuia vitendo ambavyo vimaweza kuzua mzozo.
Ikulu ya White House inasema kuwa bwana Trump amesisitiza kuwa vitendo vya Korea Kaskazini vinavuruga rasi wa Korea.
Comments
Post a Comment