BEKA ARUDI UPYA KIMUZIKI NA SPIDOCH BAND

Msanii wa muziki, Beka Ibrozama, ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Tumaini’ amejipanga na ujio wa bendi yake mpya ya muziki iitwayo ‘Spidoch Band’.


Muimbaji huyo alikuwa kimya kwa miaka 3 kuandaa bendi yake hiyo ambayo itazinduliwa Aprili 29 katika ukumbi wa Next Door Masaki Jijini Dar es salaam.
Akiongea na Bongo5 kuhusu ukimya wake na ujio huo, Beka amedai alipokuwa nje ya muziki alipata nafasi ya kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vitaboresha muziki wake.
“Beka nimerudi upya kwenye muziki tena kwa miguu miwili, nimejifunza vingi na kubwa zaidi ni ujio ya bendi yangu mpya ambayo nitaizindua hivi karibuni. Ni bendi ya muziki ambao inaendana na hadhi ya kimataifa kwa hiyo mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwaajili ya muziki mzuri,” alisema Beka.
Alisema alipotea kwa muda mrefu kimuziki kwa kuwa aliamua kujitolea muda wake wote kwaajili ya kuandaa bendi yake na kwa sasa amerudi rasmi kwenye muziki na mashabiki zake wasubiri kupata mziki mzuri kutoka kwake.

Comments