Kama ni mfuatiliaji utakumbuka October 2016, mke wa rapa Kanye West, Kim Kardashian alivamiwa na majambazi alipokuwa Paris na kuporwa vito vyake vya thamani kitu ambacho kilisababisha Kanye West aghairishe show yake iliyokuwa ikiendelea stejini na kuwaomba mashabiki radhi kwamba alipata emergency.
Taarifa zilizonifikia ni kwamba polisi mjini Paris wamewakamata watu 16 wanaoshutiwa kuwa wamehusika kwenye tukio hilo. Polisi waliwakamata majambazi wawili baada ya kukuta alama zao za vidole kwenye hoteli hiyo ya kifahari . Askari wamewashikilia kwa uchunguzi zaidi huku mdogo kabisa akiwa na miaka 22 na mkubwa akiwa na miaka 72 na kati ya hawa 16, watatu ni wanawake kwa mujibu wa polisi.
Video ya ulinzi ilionyesha watu watano kati ya hao walipoingia kwenye hoteli hiyo na kutishia mapokezi ili waonyeshwe chumba alichopo Kim Kardashian. Polisi wamewashikilia watu hao kwa ajili ya upepelezi kwa muda wa masaa 96.
Comments
Post a Comment