MRITHI WA SAMATTA ANATOKA UGANDA



January 5 2017 Abuja Nigeria ndio ilifanyika hafla ya utolewaji wa tuzo za soka za mwaka 2016 na shirikisho la soka barani Afrika Caf, tuzo hizo ambazo utolewa kwa wachezaji waliyofanya vizuri kwa mwaka husika kwa kupigiwa kura, staa wa timu ya taifa ya Algeria na timu ya Leicester City ya England Riyad Mahrez alitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika.

Mahrez alitangazwa kushinda tuzo hiyo kwa kura 361, huku Pierre-Emerick Aubameyang akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 313 wakati Sadio Mane wa Liverpool amemaliza nafasi ya tatu kwa kupata kura 186.

Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani ambayo alishinda mtanzania Mbwana Samatta kwa mwaka 2015, safari hii imerudi tena Afrika Mashariki kwa golikipa wa Mamelodi Sundowns na timu ya taifa ya Uganda Denis Onyango kushinda tuzo hiyo.



Comments