Mchezaji wa klabu ya Simba ambaye alikuwa nchini Misri akifanya majaribio ya kucheza soka la kimataifa kwenye timu ya Haras El Hodoud, Ibrahim Ajibu, amerejea nchini baada ya kumaliza siku zake za majaribio.
Ajibu ameuwambia mtandao wa Goal, kuwa amefanya vizuri kwenye majaribio yake na kwa sasa anangalia ofa kutoka kwa timu hiyo kama itamvutia anaweza kujiunga nayo.
“Nimefanya vizuri majaribio yangu na ninashukuru Mungu, kwa sababu nimekubalika sana isipokuwa sasa nasubiri ofa nzuri kutoka Haras El Hodoud, kama wakishindwa kunipa ofa nzuri nitawasubiri Kaizer Chief ambayo nayo imevutiwa na mimi na wapo tayari kunichukua,” amesema Ajibu.
Ajibu amesema kwamba anaweka mbele maslahi katika kuamua timu ya kujiunga nayo kwasababu soka ndiyo ajira yake ambayo inamfanya aweze kumudu maisha na kuendesha familia yake.
Source: Goal.com
Comments
Post a Comment