DAWA 13 ZINAZOTIBU PUMU

Pumu ni nini
Vitu vinavyoamusha pumu
Kabla tuliona namna upungufu wa maji mwilini (dehydration) unavyoweza kusababisha tatizo la Pumu mwilini, unaweza kulisoma somo hapa => Pumu ni Ishara ya mwili kuishiwa maji

Katika somo hili tutajadili dawa mbadala 13 zinazoweza kuzuia au kutibu kabisa tatizo la pumu mwilini. Chagua unayoona ni rahisi kuipata na uitumie. Unaweza kutumia dawa 2 au 3 kwa pamoja. Endelea kusoma.

Vitu vinachosababisha au kuamsha Pumu

Aleji/mzio
Tumbaku/sigara
Sabubu za kimazingira kama uharibifu wa hewa sababu ya viwanda
Uzito uliozidi
Mfadhaiko/Stress, sononeko, na huzuni
Kurithi
Maambukizi mapafuni wakati wa utotoni
Kuzaliwa mapema/njiti
Baadhi ya vyakula kama samaki, soya, mayai, korosho nk
Mazoezi
Kiungulia
Dalili za Pumu

Kupata shida wakati wa kupumua
Sauti ya kukoroma wakati unapumua
Kikohozi
Msongamano kifuani
Kujisikia umechoka wakati ukifanya kazi yoyote ya nguvu
Homa na vikohozi vya mara kwa mara
Kukosa utulivu katika usingizi


Dawa mbadala 13 zinazotibu Pumu

1. Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu

Chukua punje 5 hadi 6, menya na ukate vipande vidogo vidogo lakini siyo vidogo sana na uchemshe kwenye moto na maji kikombe kimoja (robo lita), ongeza kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi ndani yake na uache kwenye moto kama dakika 5. Ipua na unywe kwa pamoja kutwa mara 2 hadi utakapopona.

2. Tangawizi
dawa mbadala zinazotibu pumu
Tangawizi

Tangawizi pia ina faida nyingi katika mwili wako na afya yako. Tengeneza juisi robo lita yenye mchanganyiko wa tangawizi, komamanga na asali. Kunywa mchanganyiko huo kutwa mara 2 au 3 kwa matokeo ya haraka.

Namna nyingine ni kuchukua kijiko kikubwa kimoja cha juisi ya tangawizi (majimaji ya tangawizi) changanya na kijiko kikubwa kimoja cha asali na vijiko vikubwa 2 vya mbegu kavu za uwatu na uuache mchanganyiko huu kwa usiku mmoja. Kunywa mchanganyiko huu kesho yake ili kuondoa sumu kwenye mapafu yako.

3. Mafuta ya mharadali
Dawa mbadala 13 zinazotibu pumu
Mustard Oil

Chukua mafuta kidogo ya mharadali na uchanganye na kafuri (camphor) ndani yake. Jipakae mchanganyiko huu taratibu sehemu yote ya kifua mpaka uone nafuu inajitokeza. Hakikisha unayapasha mafuta kidogo katika moto kabla ya kuanza kujipaka taratibu (masaji) ili kifua kiweze kuhisi au kulipata hilo joto na hatimaye upate uponyaji kwa aharaka zaidi. Fanya zoezi hili wiki 2 hadi 3

4. Mtini (Figs)
Image result for PICHA YA FIGS
Mtini ni dawa nyingine ya asili (home remedy) nzuri dhidi ya pumu. Loweka baadhi ya mitini mikavu ndani ya maji kwa usiku mmoja. Kula huo mtini uliolowekwa kesho yake asubuhi kabla ya kula kitu kingine chochote. Pia kunywa maji hayo yaliyoloweka mtini kwa ajili ya kujitibu pumu au asthma. Fanya hivi kwa wiki 2 hadi 3

5. Mafuta ya mkalitusi
Image result for PICHA YA MAFUTA YA MKARATUSI
Mafuta ya mkalitusi (Eucalyptus essential oil) yanaweza kupelekea uponyaji wa haraka kwa mtu anayesumbuliwa na pumu. Weka matone machache ya mafuta haya ndani ya kikombe cha maji ya moto na usogeze pua yako karibu na mvuke unaojitokeza na uuvute ndani taratibu. Hii itasaidia kuzifungua pua zilizokuwa zimeziba sababu ya pumu na hivyo hewa inaweza kuanza kuingia na kutoka kirahisi zaidi.

6. Asali
dawa mbadala zinazotibu pumu
Asali

Kama unatafuta dawa ya asili ya kutibu pumu basi asali ndiyo dawa bora ya asili inayotibu pumu kuliko dawa nyingine yoyote. Unaweza kutumia kijiko kidogo kimoja cha chai kilichochanganywa na robo lita ya maji ya moto walau mara 2 mpaka 3 kwa siku au unaweza kuwa unanusa ile harufu fresh ya asali mara kadhaa kila siku.

Namna nyingine ni kuchukua kijiko kikubwa kimoja cha asali mbichi changanya na nusu kijiko kimoja cha chai cha mdalasini ya unga na ulambe mchanganyiko huo kila unapoenda kulala kila siku hadi upone.

7. Kitunguu maji
Image result for PICHA YA KITUNGUU MAJI
Vitunguu vinajulikana kuwa na sifa ya kutibu uvimbe (inflammatory) na vimethibitika kuwa na msaada mkubwa katika kusafisha njia ya hewa. Kwahiyo kama wewe ni mhanga wa pumu au asthma basi unapaswa kuwa unatumia vitunguu maji kwa wingi kila siku vikiwa vibichi kabisa, vikiwa katika kachumbali au hata vikiwa vimepikwa pamoja na mboga mboga zingine.

8. Matunda na Limau
Image result for PICHA YA LIMAORelated image

Matunda kama stroberi, bluberi, papai, na machungwa yameonyesha kuwa na msaada kwa watu wanaosumbuliwa na pumu. Pia limau zina vitamin C na zinatakiwa kutumia sambamba na maji, sukari/asali na chumvi kidogo ya mawe walau mara moja kwa siku kwa majuma kadhaa ili kujitibu ugonjwa huu wa pumu.

9. Samaki
Image result for picha ya samaki kibua
Kula mara kwa mara samaki kama ‘salmon’ (au samoni kwa Kiswahili ni samaki mkubwa mwenye mnofu mwekundu), tuna au jodari, dagaa chumvi wa baharini (sardines) kunaweza kuwa msaada mkubwa sana katika kujitibu tatizo la pumu. Samaki hawa wote huyafanya mapafu yako kuwa safi, salama na yenye nguvu katika kupambana na tatizo la pumu na kuitibu haraka na kwa ufanisi. Ingawa ikiwa hauwezi kula hawa samaki katika hali ya kupikwa basi unaweza kubadili kwa kutumia mafuta yatokanayo na samaki hawa.

 10. Zabibubata (Gooseberries/Amla)
dawa mbadala zinazotibu pumu
Zabibubata/Zabibu nyekundu

Zabibubata ni nzuri sana katika kutibu pumu. Ponda ponda zabibubata kadhaa na ongeza asali kidogo ndani yake, tumia mchanganyiko huu kila siku na ukae mbali na pumu.

 11. Mbegu za Shamari ( kiungo jamii ya karoti)
Dawa mbadala zinazotibu pumu
Shamari

Tumia mbegu za shamari kila mara ili kujitibu na shambulio la asthma/pumu.

 12. Maziwa ya moto
Image result for PICHA YA CHAI YA MAZIWA
Ongeza kiasi sawa cha mafuta ya mzeituni na asali ndani ya kikombe cha maziwa ya moto. Kunywa mchanganyiko huu pamoja na punje mbili au tatu za kitunguu swaumu kabla ya chakula cha asubuhi kwa majuma kadhaa. Dawa hii ya asili inaponya pumu kwa haraka sana.

 13. Majani ya Kotimiri
Dawa mbadala zinazotibu pumu
Kotimiri

Majani ya kotimiri (Parsley leaf) ni dawa mbadala nzuri sana kwa ajili ya kikohozi. Andaa chai ya majani haya na asali unywe kila siku. Itatibu kikohozi, itasafisha koo na kutibu pumu kadri siku zinavyosogea wakati ukiendelea kutumia chai hii kila siku.



Comments