BILL NA CLINTON KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA TRUMP


Bill Clinton na mke wake Hillary wamepanga kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Donald Trump, kwa mujibu wa ripoti.

Familia hiyo itahudhuria sherehe hizo jijini Washington, D.C. January 20 kumwangalia Trump akiapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani.

Pia Rais wa zamani wa nchi hiyo, George W. Bush ametangaza kuwa atahudhuria sherehe hizo pamoja na mke wake, Laura. Hata hivyo taarifa ya Bush imedai kuwa baba yake, George H.W., hatohudhuria kutokana na umri wake kuwa umeenda sana.

Comments