LIL WAYNE NDANI YA MAJANGA MAPYA



 Inaonekana rapper Lil Wayne atatumia muda wake mwingine ndani ya mwaka 2015 kwenye chumba cha Mahakama manake headline ya sasa ni yeye kashtakiwa na dereva wake wa zamani.
Ameshitakiwa na dereva wake wa zamani kwa kile alichosema ni kutishiwa kuuwawa tena na bunduki ikihusika, yaani kisa kilitoka siku saa tano usiku anamuendesha Lil Wayne. 

 Lil Wayne
Kilichomkasirisha Wayne ni pale dereva huyo alipoingia kwenye kituo cha mafuta kwa ajili ya kuweka mafuta, Wayne akakasirika akaikoki mpaka bunduki na kumwambia dereva, ‘nipeleke hotelini haraka, sasa hivi‘ kitisho kilichomfanya dereva huyo kuondoa gari bila kuweka mafuta.
Dereva Mark Jones anasema alikodishwa kumwendesha Lil Wayne na timu yake kwenye ziara ya kimuziki mwaka 2014 na sasa kaamua kumshitaki Mahakamani.

Comments