WOLPER NA WASTARA KIMENUKA

Mtazamo:Ukistaajabu ya Kajala na Wema, utayaona ya Wastara na Wolper
 Kweli nimeamini samaki mmoja akioza wote huoza, hadi wewe wastara? Hukumbuki wolper alivyohangaika na marehemu mume wako? Dada wa watu akajitolea mamilion ili mume wako akatibiwe India? Umesahau wema wote hadi ukalia nachozi na kumuona wolper ni Mungu mtu?

Pesa tu ndio zinakutoa utu na kukufanya uumize moyo wa mwanamke mwenzio aliyejitolea wakati una shida ili aokoe maisha ya mume wako kipenzi japokuwa haikuwezekana (Mungu ailaze roho ya marehemu peponi ), inasikitisha na kuumiza sana, kuna watu wa kufanya huu unyama ila sio wewe wastara.

Unadhani wolper atakuwa anakufikiliaje? Achilia mbali mapungufu yake mengine, ata kama waliachana haileti picha nzuri kuwa na mahusiano na ex wa wolper, bora angefanya mtu mwingine lakini sio wewe, hakuna mtu unayepaswa kumheshimu kama wolper, ni kama ndugu yako.

Mbaya zaidi huyo Mchumba wako ambae mnadai mnataka kuoana anamtolea maneno machafu wolper eti alikuwa anapiga sana mzinga anaomba mpaka elfu 20 na ana tabia chafu, ivi unajisikiaje? Ila kumbuka muosha huoshwa.

Comments