Mtoto muathirika wa utesaji nyumbani
Picha
ya kushtusha imeachiliwa kwa ulimwengu hivi karibuni picha
inayomuonesha mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitano aliye kondeana
,aliyetelekezwa katika sehemu ya chini ya nyumba yao ,aliyefungiwa na
kuachwa afe njaa na familia yake.
Tammi
Bleimeyer,mwenye umri wa miaka 33,na mumewe Bradley,mwenye miaka 24,
wameshtakiwa kwa kosa la kuhatarisha uhai wa mtoto wao baada ya kumkuta
mtoto huyo akiwa katika hali dhoofu katika majira ya baridi ,kitongoji
cha Harris, huko Texas.
Askari
aliye fanikisha kupatikana kwa mtoto huyo Mark Herman,amesema kwamba
amefanya kazi ya polisi katika kipindi cha miaka thelathini lakini
hajawahi kushuhudia tukio lanamna hii.
Askari
huyo anasema wamemkuta mtoto huyo katika hali mbaya ana njaa
kali,amekondeana,amevilia damu mwilini kama aliyekuwa akipigwa ama
kupitia mateso makali na ngozi yake ilionekana kama imeachana na mifupa
,ilikuwa ni hali ya kutisha sana kumwona mtoto katika hali hiyo.
Bradley
alikuwa akibishana na mtoto huyo wa kambo mwenye umri wa miaka kumi na
sita aliyekuwa akiwataka wazazi wa mtoto huyo kuacha kumfungia mtoto
wako katika chumba cha chini ya ardhini nyumbani mwao .
Na
polisi walipofika nyumbani hapo waligundua chumba kidogoo,chini ya
nyumba hiyo kikiwa kimefungwa na godoro tu ndani yake na mtoto aliyeketi
juu ya godoro ,ingawa mama wa kambo wa mtoto huyo alimtorosha baada ya
kujua kwamba polisi wanamfuatilia, na kumkuta katika chumba cha hoteli
na kumfuatilia hatimaye kumchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitalini
kwa matibabu.
Ingawa
mpaka mtoto huyo anafikishwa hospitalini, sababu za kufungiwa kwa mtoto
huyo hazikufahamika mara moja ,na wazazi wa mtoto huyo wamekataa
kuzungumzia tukio hilo .
Baba
wa mtoto huyo anashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, na mtoto
wake bado amesalia hospitalini kwa matibabu zaidi katika hospitali ya
watoto iliyoko mjini Texas
Via>>BBC
Comments
Post a Comment