Mwanamke mmoja Michelle katika jimbo la Corolado Marekani amepoteza kichanga chake baada ya mwanamke mmoja kumchoma kisu tumboni na kuchukua kichanga chake kilichokuwa na miezi saba.
Dynel Catrece Lane ndie mwanamke ambaye ametajwa kuhusika na kosa hilo, alimchoma mwanamke huyo kisu tumboni na kumtoa kichanga hicho halafu akakimbia kwenda Hospitali akidai kwamba ametokwa ujauzito, wakati huo alikuwa amekishika kichanga hicho mkononi kikiwa kimefariki.
Dynel Catrece Lane
Baada ya Lane kufanya tukio hilo na kukimbia, Michelle alipiga simu ya dharura 911 kuomba msaada; “amenichoma tumboni.. nina ujauzito..“
Comments
Post a Comment