UBAGUZI WA RANGI WAMTOA MCHEZAJI WA NIGEIA HUKO UTURUKI


Mshambuliaji wa Emmanuel Emenike wa Fenerbahce amekuta akishindwa kujizuia na kulazimisha afanyiwe mabadiliko na kutolewa nje hata kabla ya kipindi cha pili.Katika mechi hiyo ya Ligi kuu ya Uturuki dhidi ya wapinzani wao Besiktas, Emenike raia wa Nigeria alilazimisha kutoka na kuvua jezi wakati mashabiki walipoanza kumshambulia kwa maneno makali yakiwemo ya kibaguzi.  


Mashabiki hao walikuwa wakimzoea baada ya kushindwa kutuliza mpira mrefu aliopigiwa.

Hali hiyo ilionyesha kumuudhi ingawa mashabiki hao pia walilalama kwamba msimu huu amekuwa hana msaada kwa timu yao. 

Pamoja na kufanikiwa kutoka, Emenike alirudishwa na benchi la ufundi akiwemo kocha wa timu hiyo ambaye hata hivyo baadaye alilazimika kumtoa baada ya kipindi cha kwanza kwisha.

Ubaguzi wa rangi umekuwa ukiendelea katika nchi mbalimbali ikiwemo Uturuki ambayo ndiyo nchini pekee duniani iliyo katika mabara mawili ya Asia na Ulaya.

Asilimia kubwa ya Waturuki ni wale wenye asili ya Waarabu, lakini ajabu nao wamekuwa na tabia hizo mbovu za kishenzi za ubaguzi wa rangi.
 

Comments