Imekuwa kama desturi kwa mastaa wa Nigeria mara wanapofiwa na watu wao wa karibu kukaa muda mrefu bila kuwazika, ilianza kwa nyota P-square kuchelewa kumzika mama yao Josephine Okoye ambaye alifariki May 11 2012 na kuzikwa Agust 2 2012 akafuatiwa na baba yao Moses Okoye ambaye alifariki Novemba24 na kuzikwa January30.
Matukio hayo yaliacha maswali kwa watu
mbalimbali na kusababisha kuingia kwenye headlines za vyombo mbalimbali
vya habari duniani.
Safari hii ni kwa staa mwingine Yemi Alade ambaye baba yake mzazi kamishna mstaafu wa polisi J.A Alade ambaye alifariki January 16,2015 sasa anatarajiwa kuzikwa May7 mwaka huu.
Yemi Alade alisema baada ya kumaliza
ziara zake Ulaya atarudi na kuanza maandalizi ya kumzika baba yake
lakini hakuweza kueleza ni wapi shughuli hiyo itafanyika.
Comments
Post a Comment