Ikiwa leo ni siku ya UKIMWI, Duniani ambapo Tanzania Kitaifa siku hiyo inafanyika Mkoani Njombe Juhudi za kupambana na maambukizi ya ukimwi mkoani humo zimezidi kushika kasi kutoka katika mashirika mbalimbali na kuanza kuungana na viongozi wa mila ili kutokomeza mila hatarishi.
Akizungumza na East Africa Radio katika viwanja vya Sabasaba mkoani njombe, afisa uhusiano wa PSI kanda ya nyanda za juu kusini, Sanday Beebwa amesema kuwa katika vitu vinavyo ongeza kasi ya maambukizi mkoani humio na Tanzania kwa ujumla ni pamoja na tamaduni na mila.
Maadhimisho haya ambayo kilele chake ni leo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Comments
Post a Comment