Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania bila ubishi wowote ndio klabu bora kwa sasa ulimwenguni kote , hii ni kutokana na aina ya matokeo ambayo wanayapata kwneye mashindano mbalimbali ambayo wanashiriki kuanzia ligi ya Hispania , Kombe la Mfalme , Ligi ya mabingwa barani ulaya na michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko nchini Morocco ambako mabingwa hao wa Ulaya wameingia hatua ya Fainali .
Jumla yote Madrid imeshinda michezo 21 katika mashindano yote rekodi ambayo wanazidi kuivunja huku kukiwa hakuna dalili zozote za timu hii kupata matokeo tofauti na ushindi huku wakiwa wamevunja rekodi ya kushinda mechi 18 mfululizo iliyowahi kuwekwa na Barcelona iliyokuwa chini ya Mholanzi Frank Rijkaard katika msimu wa mwaka 2005/06.
Kwa kasi hii rekodi pekee ya kushinda mechi mfululizo iliyobaki kuvunjwa itakuwa ile iliyowahi kuwekwa na Ajax Amsterdam kwenye msimu wa mwaka 1971/72 ambapo timu hiyo ilishinda michezo 26 .
Ubora huu unaonekana kwenye matokeo unatokana na aina ya wachezaji ambao Real Madrid inao wakiongozwa na mchezaji bora kwa sasa Cristiano Ronaldo .
Takwimu kadhaa zinaonyesha kuwa Real Madrid wamekuwa bora kwenye kila idara na ni vigumu sana kuwazuia .
Katika michezo 21 ambayo timu hii imecheza hadi kufikia sasa , imefanikiwa kufunga jumla ya mabao 79 , ikiwa imeruhusu kufungwa mabao 10 pekee .
Katika mabao hayo 79 ambayo Madrid imefunga jumla ya mabao 19 yamefungwa kwa kutumia mguu wa kushoto , mabao mengine 42 yakiwa yamefungwa kwa kutumia miguu ya kulia na mengine 15 yakiwa yamefungwa kwa kicha .
Zaidi ya hapo , mabao 9 yamefungwa nje ya eneo la hatari au kisanduku cha penalty (penalty box) na mabao 70 yakiwa yamefungwa ndani ya eneo hilo na mabao 8 yamefungwa kwa njia ya adhabu ya mkwaju wa penati .
Katika kipindi hiki chote wachezaji kadhaa wamechangia katika mafanikio ambayo Real imeyapata kwenye michezo yake 21 ambayo imeshinda mfululizo kuanzia kwa Cristiano Ronaldo , Gareth Bale , Karim Benzema , James Rodriguez , Toni Kroos, Isco ,Sergio Ramos , Pepe ,na kipa Iker Cassillas ambaye hatimaye amerudisha hadhi yake iliyowahi kutishia kupotea chini ya kocha Jose Mourinho .
Nyuma ya mafanikio yote haya ni kocha Mtaliano Carlo Ancelotti ambaye amefanikiwa kuwafanya wachezaji wote wa Real Madrid kuwa kitu kimoja na kupambana mwanzo mpaka mwisho kuhakikisha wanatimiza lengo ambalo ni kujaribu kuibuka na ushindi kwenye kila dakika 90 wanazokuwa uwanjani dhidi ya wapinzani wa aina tofauti .
Kocha Mtaliano Carlo Ancelotti amefanya kazi kubwa ya kuifanya Real Madrid kuwa timu bora barani Ulaya .
Kocha Mtaliano Carlo Ancelotti amefanya kazi kubwa ya kuifanya Real Madrid kuwa timu bora barani Ulaya .
Tarehe Mpinzani(timu) Mashindano Magoli(real) Magoli(wapinzani) Umiliki Mpira Ufasaha wa pasi Pasi Mashuti
16/09/14 Basle Champions League 5 1 54.35 90.36 560 17
20/09/14 Deportivo la Coruna La Liga 8 2 59.83 91.75 679 15
23/09/14 Elche La Liga 5 1 64.74 90.91 660 20
27/09/14 Villarreal La Liga 2 0 49.72 85.66 502 7
01/10/14 Ludogorets Champions League 2 1 60.93 87.77 548 15
05/10/14 Athletic Bilbao La Liga 5 0 60.12 86.76 589 19
18/10/14 Levante La Liga 5 0 61.3 90.72 636 17
22/10/14 Liverpool Champions League 3 0 54.17 88.38 680 12
25/10/14 Barcelona La Liga 3 1 42.19 85.38 431 11
29/10/14 Cornella Copa Del Rey 4 1 73.22 89.58 758 11
01/11/14 Granada La Liga 4 0 66.77 88.06 628 15
04/11/14 Liverpool Champions League 1 0 60.13 90.99 710 15
08/11/14 Rayo Vallecano La Liga 5 1 43.83 81.38 435 15
22/11/14 Eibar La Liga 4 0 62.3 85.51 559 17
26/11/14 Basle Champions League 1 0 53.32 84.35 543 6
29/11/14 Malaga La Liga 2 1 57.86 88.4 474 18
02/12/14 Cornella Copa Del Rey 5 0 63.08 89.71 680 10
06/12/14 Celta Vigo La Liga 3 0 48.78 81.75 389 17
09/12/14 Ludogorets Champions League 4 0 61.77 91 600 19
12/12/14 Almeria La Liga 4 1 60.5 79.91 458 12
16/12/14 Cruz Azul FIFA Club World Cup 4 0 58.28 89.16 609 20
Comments
Post a Comment