MWANAMKE AMTUPA MTOTO DIRISHANI KWENYE BASI

SAMSUNG
 Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sedoyeka amesema Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mjukuu wake ambapo alimtupa mtoto huyo kwenye dirisha la basi ambalo lilikuwa kasi, mwanamke huyo Waridi Saidi alimtupa mtoto huyo akiwa kwenye basi namba T 981 ALS  la kampuni ya  Salumu Classic lililotoka Dar kwenda Kigoma.
Mama huyo alimtupa mtoto huyo kijiji cha Iguguno, wilaya ya Mkalama alimtupa mjukuu wake Mayasa Meshaki, Dk  Adamu Hussein amesema  walimpokea mtoto akiwa katika hali mbay kutokana na kuvuja damu nyingi na siku ya pili alifariki  dunia  kutokana na jeraha la kupasuka kwa fuvu la kichwa.
 SAMSUNG
 Lawaridi amesema; “dirisha lilikuwa wazi yani nilimshusha tu nikamchukua Mayasa nikamtupa bila kutegemea… Watu wakanivamia sasa huku wanapiga kelele kuanza kunipiga… Wamenipiga sana tu, basi gari ikasimama wakawa wameenda kumtafuta mtoto… nikaambiwa mtoto amepatikana lakini mpaka dakika hii sijamuona...“
 SAMSUNG

Comments