PAPAA MSOFE KUSHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI....KISA...


Papaa Msofe akiingia chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. (Picha na Maktaba yetu)
MFANYABIASHARA anayekabiliwa na kesi ya mauaji, Marijan Abubakar, maarufu kama Papaa Msofe leo ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kusikiliza kesi yake baada ya kuugua.
Papaa Msofe na mwenzake, Makongoro Joseph, wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya Onesphory Kitoli, wataendelea kusota rumande baada ya kesi hiyo kuahirishwa mpaka Novemba 18, mwaka huu itakaposikilizwa kuvuta subira ili upelelezi ukamilike.

Comments