MSANII WA BONGO MUVI APEWA KIPONDO NA BABY WAKE KISA HIKI


Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan akiwa na jeraha la kipigo kutoka kwa hawara yake.
STAA wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan, hivi karibuni alionja joto ya jiwe baada ya kushushiwa kipigo kizito na hawara wake aliyetajwa kwa jina moja la Ally.Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio Tiko alikuwa na Ally nyumbani kwake,
Mwananyamala ndipo ghafla hali ya hewa ikachafuka baada ya pedeshee mmoja kumpigia simu mwigizaji huyo.
“Mzozo ulianzia kwenye simu na huwezi amini amemvunjia simu yake kwani alimpiga kwa sababu alikuwa akiongea na mwanaume mmoja kimahaba na hapo ndipo timbwili lilipoanza,” kilidai chanzo hicho.


Kikazidi kumwaga ubuyu kwamba, wakati kipigo cha ngumi kikiendelea, mwanaume huyo alimrushia chupa Tiko ambayo ilimpasua usoni na kumuacha na jeraha kubwa lakini hakwenda kumshtaki polisi kwa kuwa anampenda sana.
Tiko Hassan akiuguza jeraha lake.
Baada ya habari hizo kutua gazetini, mapaparazi wetu walimtafuta Tiko na kufanikiwa kumpata nyumbani kwao Mbagala ambapo alifunguka:
“Yule ana wivu sana na mimi, huyo mtu aliyenipigia simu simjui na alikuwa akijaribu kunitongoza na mimi nilikuwa nikimkaripia lakini kibao kilinirudia, nikapigwa.
“Nilitibiwa katika Hospitali ya Cam hapa Mbagala, kwa sasa nauguza kidonda nikipona nitajua cha kumfanyia kwani amenifanya niwe na jeraha usoni.”

Comments