HII NDO SABABU KUBWA YA WEMA KUMBWAGA DIAMOND

MISS Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amevunja ukimya kwa kuamua kuanika kisa cha yeye kummwaga aliyekuwa mwandani wake, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Akizungumza na Amani katika mahojiano maalum jijini Dar, juzikati, Wema alianza kwa kufunguka kwamba, kuna watu wamekuwa wakizungumzia ishu ya yeye kumtema Diamond huku kisa wakiwa hawakijui na wengine wamehamishia sababu kwa nyota wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’, jambo ambalo si kweli.
Wema alimwaga ‘ubuyu’ kwamba, yeye ameamua kumpa likizo ndefu Diamond ili kila mmoja aweze kufanya mambo yake ya maana kwa uhuru mkubwa hasa baada ya jamaa huyo kunukuliwa na magazeti pendwa akisema hana mpango wa kuoa jambo ambalo lilimkatisha tamaa na kumwacha njia panda.
SAFARI YAKE CHINA NAYO TATIZO
Kuhusu suala la kusema amempa likizo ndefu ili kila mtu afanye mambo yake,
Wema alirejea safari yake ya China hivi karibuni ambapo Diamond hakutaka asafiri ila akalazimisha. Hapo aliona anatakiwa kuwa huru zaidi.

Wema Isaac Sepetu  akipozi kimahaba na 'Diamond Platinumz'.
MWISHO WA LIKIZO
Wema alipotakiwa kutaja mwisho wa likizo hiyo endapo ni ya siku 28  kama ilivyo
kwa sheria ya kazi ya Tanzania, aligoma kusema chochote huku akisisitiza amempa likizo Diamond.
AMZUNGUMZIA ZARI
Staa huyo asiyekaukiwa na matukio, alikwenda mbele zaidi kwa kumzungumzia Zari ambapo alisema kuna wanaodai mwanamuziki huyo tajiri yuko kimapenzi na Diamond, lakini yeye haoni ukweli wowote kwani anajua wawili hao wana ‘projekti’ ambayo ni mawazo ya muda mrefu.
BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA
“Kwanza naomba watu wajue kuwa, projekti ya Diamond na Zari ninaijua na bahati nzuri Zari ni shoga‘ngu tangu kitambo hivyo yote yanayofanyika mimi nayatambua hatua kwa hatua pamoja na kwamba sijaongea na Diamond siku nyingi,” alisema Wema.

Diamond akiwa na Wema Isaac Sepetu siku ya bethidei yake.
DIAMOND AULIZWA KAMA ANAITAMBUA LIKIZO NDEFU
Baada ya mazungumzo na Wema, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond kwa lengo la kutaka kumfahamisha kama anafahamu kwamba amepewa likizo ndefu.
“Dah! Nashindwa niseme nini hapo! Lakini ujue maisha kila mfa maji siku zote haishi kutapatapa, kiukweli mimi hapo naona Wema anatoa majibu ya kisiasa tu.
“Nashindwa kujibu kila linalosemwa na watu ila kuna kipindi mtu hutakiwi kujibu kila kitu. Kuna mambo mengine yanatakiwa uyaache yapite tu.
“Mimi nimeachwa na Wema, Zari ni rafiki yangu tu, acheni projekti iendelee,” alisema Diamond huku akichekacheka kwa ishara ya furaha akijiandaa kuachia ngoma kali mpya iitwayo ‘Nitampata Wapi’ leo.

Hii ni picha ya mwisho ya wawili hao kuonekana pamoja.
KWENYE WHATSAPP
Wakati Diamond akisema hayo, baadaye kwenye maelezo yake mafupi (profile) ya WhatsApp aliweka picha ya Zari huku akiambatanisha na maneno yaliyosomeka:
“Unapokosa usisikitike, Mwenyezi Mungu kakuandalia kizuri zaidi.”
Wema na Diamond wamekuwa na kasumba ya kuachana na kurudiana hivyo kuna kila dalili wawili hao wakarudiana tena.

Comments