SOME FEW INTERESTING FACTS ABT PROPHET ELIAH mungu wa majeshi.!
Baada ya kifo cha aliyekua kiongozi na muasisi wa Kanisa la Pool of Siloam Nabii Eliya mungu wa Majeshi a.k.a Adamu wa pili, gazeti la JIBU YA MAISHA linalomilikiwa na kanisa la TAG la tar.16 November 2014, limeandika mambo machache ya kushangaza kuhusu kiongozi huyo na kanisa lake hilo maarufu hapa nchini. Nami nanukuu kwa maslahi ya umma:
1. Idadaiwa sababu ya kifo chake ni kuchomwa na msumari mkononi na akakataa kwenda hospitali kwa sababu kanisa hilo haliamini ktk tiba za hospitali. Pia wanaamini hamna kuugua na Nabii Eliya aliwashuhudia kuwa hajawahi kuugua tangu azaliwe).
2. Nabii Eliya alijiita Mungu wa Majeshi (kinyume na maagizo ya MUNGU wa kweli ambaye hagawani utukufu na wanadamu). Lakini nabii Eliya aliwahi kusema hatakufa na hata alipokufa waumini wake wanaamini hajafa bali amepaa mbinguni. (wengine wameanza kushuhudia kuwa walimuona akipaa, na kuwa eti mwili wake utakaozikwa ni taswira tu, ila mwili wake halisi amepaa nao mbinguni).
3. Nabii Eliya alikua anasema anaishi mbingu ya saba na hapa duniani kilichopo ni taswira yake tu.. ila yeye yupo Mbingu ya 7 na huwa anawahudumia wafuasi wake akitokea huko mbingu ya 7.
4. Alikataa matumizi ya neno BIBLIA kanisani kwake. Alitoa kava za Biblia na kuweka kava zake zenye maandishi "Kitabu cha haki"
5. Alipinga kuwa siku za mwezi si 30 bali 28 na akatengeneza Kalenda yake yenye siku 28 inayofuatwa na waumini wake wote.
6. Mwaka 2008 alipanga upya majira ya mwaka na kuonesha kuwa mwanzo wa mwaka si January bali March (Wao huita Aviv) na mwisho wa Mwaka si December bali February (wao huita Adari).
7. Wanaamini Sikukuu ya Chrismass (kuzaliwa kwa Kristo) sio tar.25 December bali tar.28 February.
8. Unapokua muumini wa kanisa hili hulazimika kubadili majina yako yote maana wanaamini yana laana hivyo hukupa majina mengine.
9. Waumini wa kanisa hili wanapomsalimia mtu asiye muumini wao kwa kushikana mikono hushauriwa kunawa mikono haraka sana baada ya salamu, ili kuondoa mapepo yanayoweza kuwapata kwa kushikana mikono.
10. Waumini wa kanisa hili wanaamini SHETANI HAYUPO.. Shetani alishakufa. Na aliyemuua Shetani ni Nabii Eliya.. Wanaamini kuwa tar.4 Novemver 2008 Nabii Eliya alimkamata shetani akampiga kabali na kumuua.. Hivyo Shetani hayupo hai tena..
Huyo ndo Adamu wa pili Nabii Eliya, Mungu wa Majeshi ambaye majina yake halisi mi NDUNAMINAMFOO MUNUO, Mchagga wa Moshi Machame.. Nafasi yake ya uongozi wa kanisa imechukuliwa na mtu mmoja ajiitaye "Kuhani Eliya Miaka Elfu moja.!"
R.I.P NDUNAMINAMFOO MUNUO.!!
Comments
Post a Comment