AGNESS MASOGANGE MATATANI TENA


 Video model Agnes Masogange mwaka jana alitawala vyombo vya habari baada ya kukamatwa na polisi huko South Africa akiwa na mwenzake Melisa Edward wakiwa na mzigo wa Crystal Methamphetamine wenye thamani ya Tsh bilioni 6.8.
Taarifa mpya kutoka kwa kamanda wa polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya Gedfrey Nzowa inasema kikosi hicho kilimshikilia Masogange usiku wa juzi baada ya kurejea akitokea South Africa. Taarifa inasema kwamba Masogange alihojiwa kwa zaidi ya masaa 10 na kupekuliwa na baadae kuachiwa huru bila masharti.

Comments