WEMA ATAMPA ZAWADI GANI DIAMOND...SOMA HAPA

Diamond Happy_full
Leo, Octber 2, Staa wa muziki wa bongo flava Nasibu Abdul aka Diamond anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza umri wa miaka 25.
Mpenzi wake, Wema Abraham Sepetu ambaye huenda wengi wanasubiri kusikia atasema nini au atatoa zawadi gani kwa Diamond ambaye alimpa gari aina ya Nissan Murano, ameandika machache kwenye Instagram na kueleza kuwa anajipanga kuandika ujumbe mzuri zaidi.
“Happy Birthday to you my original soul… ngoja nitulie kwanza ndo niandike caption maana nina mengi kwa kweli… ila jua nakupenda sana…” Ameandika Wema.
 
Tuendelee<br /> kusubiri kitatokea ninI pale Golden Jubilee Towers, Dar ambapo sherehe<br /> ya siku ya kuzaliwa ya Diamond itafanyika na tayari wageni maalum<br /> wameshaalikwa.
Naye Shetta ameamua kumlipa fadhira ya shukurani Diamond Platinumz kwa mchango wake kwenye maendeleo ya muziki wake ikiwa ni sehemu ya kumtakia heri ya siku Shetta ameandika kwenye Instagram:
“Kwenye maisha Kila mtu ana watu wake ambao ni muhimu sanaaaa huenda wamefanya vitu vingi,huenda ikawa ushauri au kupigania kwa njia yoyote ile kuhakikisha mafanikio ya mtu fulani japo hata asilimia ndogo,nisiwe muongo Naseeb katika watu ambao wamekua kwenye sehemu kubwa katika kazi zangu na issue zingine za kawaida katika kipindi kirefu sasa… Mimi namuonaga zaidi ya ndugu na sio rafiki tenaaa kwa vile tulivyoishi na tunavyoendelea kuishi mpaka sasa…back 2 the point Mwaka 1989 mwezi na tarehe kama ya leo huyu jamaa Alizaliwa,so leo ni siku yake muhimu Naomba mnisaidie kumuwish #HAPPYBIRHTDAY Mr Dangote Inshallah M/mungu Azidi kuleta kheri na baraka nakutakia maisha marefu #BabaQayllah cc @diamondplatnumz”

Comments