UWOYA AMKANA MSAMII


Uwoya
Star wa filamu mwenye jina kubwa nchini Tanzania Irene Uwoya amesema kuwa hana uhusiano wa kimapenzi naMsami ambaye ni moja wa wakufunzi wa Tanzania House Of Talents(THT) kwa upande wa dancers.
Akizungumza na Bongo5 Irene amesema kuwa ukaribu wake na Msami ambao ulizua habari kuwa ni wapenzi ulitokana na kufanya wote filamu ya inayoitwa Kigoda ambayo inahusu drama na muziki hivyo Msami kushiriki. Uwoya amesema kuwa filamu yake mpya hiyo imegharimu pesa nyingi na baadhi ya scenes zimeshutiwa nchini S.Africa ili kuleta ladha mpya ya locations tofauti tofauti.

"Msami sijawahi kuwa na mahusino nae, alikuwa kama msanii mwenzangu, hata ule ukaribu wake na mimi ambao ulizua tetesi za kuwa na mahusiano nae ni kutokana na hii filamu, kwahiyo watu wajue ni kazi tu" Uwoya aliiambia Bongo5

Na kuongeza kwa kusema "filamu ya Kigoda ni filamu ya aina yake katika filamu ambazo nimewahi kuzifanya, filamu inahusu drama na muziki, imeshaghaimu pesa nyingi sana, ndani utaona watu wakicheza muziki na maisha ya wasanii kwa hiyo itakuwa tayari hivi karibuni, tutatangaza ikiwa tayari kwenda sokoni

Comments