Wapenzi huambiana ‘Chora Tattoo ya jina langu nijue unanipenda sana’ ila baada ya muda wapenzi wengi hujutia jambo hili na kutumia nguvu nyingi kufuta au kufunika tattoo hio na picha nyingine ambayo hawakutegemea kuchora. Miaka kadha iliyopita Nick alichora tattoo ya jina la Mariah mgongoni kama ishara ya mapenzi ya kweli ka mke wake ila juzi kwenye club inayoitwa Playhouse Nightclub mgongo wa Nick ulionyesha picha nyingine ambayo imeripotiwa kuwa ni ya Yesu akiwa msalabani na mabawa ya malaika yakiwa pembeni mwake.
Comments
Post a Comment