MWANAMUZIKI mwenye vituko kila kukicha Bongo, Baby Joseph Madaha, ametoa dukuduku lake la moyoni na kusema kuwa kila kukicha anayatamani mapenzi ya Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ kama angekuwa yeye.
Akizungumza na paparazi wetu, Baby alisema kuwa kila akiwaona Wema na Diamond anatamani sana na yeye awe kwenye uhusiano wenye kupendwa na kuhamasisha kama ulivyokuwa wa mastaa hao kiasi ambacho amefikia hatua ya kuwaonea wivu.
“Kiukweli nikiwaona hawa watu nasikia mpaka wivu na kuna wakati natamani niwe mimi jamani maana sifikiri kama kuna ‘kapo’ kali hapa Bongo kama hii jamani, naitamani hadi basi,” alisema Baby.
Comments
Post a Comment