
Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa High Spirit uliopo Jengo la IT Plaza, Posta jijini Dar ambapo kulikuwa na uzinduzi wa huduma mpya ya mtandao wa Airtelhuku mastaa mbalimbali na waandishi wa habari wakijumuika pamoja kuanzia saa 1:00 usiku.
Mapema kabla ya uzinduzi huo, AY aliyekuwa amepiga pamba nyeusi alikuwa wa kwanza kutinga ukumbini hapo akiwa ameongozana na Mtangazaji wa Show ya Mkasi kupitia EATV, Salama Jabir.Wakiwa wanapiga stori za hapa na pale, mara Jide naye alitinga ukumbini hapo ambapo jicho lake lilitua kwa AY na kusogea karibu kwenda kusalimiana naye.

Comments
Post a Comment