HUYU NDIYE MWANARIADHA ALIYEFARIKI DUNIA

Mula
Mbulaine Mulaudzi ambaye alikuwa mwanariadha mahiri nchini Afrika Kusini amefariki kwa ajali akiwa safarini kuelekea Johannesburg kushiriki kikao cha wanariadha.
Rais wa chama cha kimataifa cha riadha (IOC) Thomas Bach amesema Mulaudzi alikuwa mwanariadha wa pekee ambapo anatajwa kuwa mmoja ya wanariadha na wanamichezo ambao Afrika Kusini itaendelea kuwaenzi kwa mchango mkubwa alioufanya kuiinua nchi hiyo katika ramani ya michezo. .
Mulaudzi amewahi kushinda medali mbali mbali kama inavyooneshwa hapa:-
2002 –Alishinda medali ya Dhahabu mashindano ya jumuia ya madola
2003 –Alishinda medali ya Shaba
2004 –Alishinda medali ya Dhahabu mashindano ya michezo ya ndani
2006 –Alishinda medali ya Fedha mashindano ya michezo ya ndani
2008 –Alishinda medali ya Fedha mashindano ya michezo ya ndani
2009 –Alishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya dunia ya mita 800
Mulaudzi alitangaza kustaafu riadha mwaka 2013, japo aliendelea kujihusisha na masuala ya riadha mpaka kipindi ambacho amefikwa na umauti saa chache zilizopita.

Comments