Mchezaji mstaafu wa timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho amehamia Queretaro ambayo ni klabu ya Mexico. Ronaldinho aliyemaliza mkataba wake na klabu ya Brazil ‘Atletico Mineiro’ mwezi wa saba amekubali mkataba wa miaka miwili na Queretaro. Ronaldinho mwenye miaka 34 amesema ‘Nimekubali kwenda Mexico sababu ya mapenzi yao kwangu na nimehamasika kuichezea Queretaro’.
Ronaldinho alishinda Champions League akiwa na Barcelona mwaka 2006,pia ameichezea Paris St-Germain na AC Milan.Alishinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2005.
Comments
Post a Comment