Kutoka Lindi kuna taarifa ambayo imethibitishwa pia na kamanda Mpinga kuhusu ajali iliyotokea Mtwara ambayo imehusisha gari la Jeshi la Wananchi Tanzania(Jwtz)imeripotiwa asubuhi ya leo na shuhuda wa eneo hilo.
Msafara huo wa Wanajeshi ulikuwa ukitokea Mtwara kuelekea Nachingwea kwenye camp kubwa ya Jeshi na ajali hiyo imetokea maeneo ya Mnolela kijijini Lindi,kwa mujibu wa shuhuda ambaye ametoa taarifa hii kupitia kipindi cha Power Breakfast kutoka Clouds Fm amesema ajali hiyo imeua wanajeshi 3 na mwenye nyumba mmoja ambaye ni mwanamke alikua kalala ndani.
Madhara mengine yaliyotokana na ajali hii ni nyumba mbili kuharibika vibaya,majeruhi wa ajali hii wamepelekwa kwenye hospital ya Mkoa wa Mtwara.
Comments
Post a Comment