KAJALA APAGAWA NA FEDHA, ATOA KUFURU YA MWAKA


Staa wa filamu, Kajala Masanja ‘K’ akiwatunza wakali kutoka Yamoto Band.
FEDHA mwanaharamu! Katika hali ya kushangaza, staa wa filamu ambaye fedha imemtembelea kwa sasa, Kajala Masanja ‘K’ amenaswa akimwaga fedha kama amechanganyikiwa mbele ya kadamnasi, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilitokea hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar, kulipokuwa na uzinduzi wa filamu ya Mateso Yangu Ughaibuni ambapo muigizaji huyo alionesha jeuri ya fedha baada ya kupagawishwa na sebene la Yamoto Band.
Awali, paparazi wetu alimshuhudia Kajala akitinga viwanjani hapo akiwa ameongozana na wapambe takriban 15 na kwenda kukaa katika meza moja ambapo mhudumu aliwasikiliza kujua wanachokunywa.
Kutokana na uzinduzi huo kutokuwa na pombe, K aliamuru kila mtu aletewe kile anachokihitaji halafu bili yote apelekewe yeye, Mama la Mama kama wanavyowaita watoto wa mjini.
“Waletee hawa vinywaji wanavyojisikia kunywa pia wasikilize meza ile pale kisha bili niletee mimi,” alisikika Kajala.

Comments