Mfahamu kijana huyu aliyekulia nchi za Europe na sasa yuko nchini tayari kabisa kushirikiana na wote katika kiwanda hiki cha burudani,
Yeye ni "Producer" mtayarishaji wa muziki na mwenye taaluma hiyo kwa muda usiopungua miaka saba sasa,ameshafanya kazi na wana muziki kibao alipokuwa Finland na England ukiwemo wimbo huo ambao atauzindua rasmi siku hiyo ya jumapili kwenye "Lovers Rock" kipindi kinacho ongozwa na "Baba T" wa eastafrica radio kinachoruka kila siku ya Jumapili saa sita mchana mpaka saa tisa alhasiri,
Hivi sasa Hashim aka Hash MotherLand amefungua Recording Studio ambayo iko Sinza jirani kabisa na Lion Hotel na yuko njiani kuachia tracks nyingine kali alizofanya hapo ikiwemo "Mahaba Niue - Baby Madaha na Fikra pana - Saigon 19 ambayo tayari yenyewe inapatikana katika mitandao ya kijamii.
Kwa habari zaidi huyu jamaa na Burudani zote jenga tabia ya kupitia hapa kwenye blog yetu.
Comments
Post a Comment