Mchezaji mpya wa klabu ya Manchester United Angel Di Maria amezungumzia juu ya uhamisho wake kutoka Madrid na huku akisema kwamba isingekuwa mmoja wa marafiki zake kwenye klabu ya Snatiago Bernabeu basi angeweza kuihama timu hiyo msimu uliopita.
Di Maria amejiunga na Manchester United mapema wiki iliyopita kwa ada ya uhamisho wa £59m ambayo imeweka rekodi mpya nchini Uingereza
Winga huyo wa kimataifa wa Argentina ambaye tayari alishaanza kuhususishwa na uhamisho wa kutoka Real wakati wa dirisha la usajili la msimu uliopita, lakini baadae aliendelea kubaki Santiago Bernabeu kwa sababu ya mchezaji Cristiano Ronaldo, abaye kwa mujibu wa Di Maria ni marafiki sana.
“Ukweli ni kwamba nina mahusiano mazuri mno na Cristiano Ronaldo na nilibaki Madrid msimu uliopita shukrani kwa Ronaldo,” Muargentina huyo aliiambia ESPN Radio.
Di Maria ameshaanza kuitumikia Manchester United ambapo alianza kwenye mechi ya ligi kuu ya England dhidi ya Burnley.
Comments
Post a Comment