Baba mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Kaga mkazi wa Mwanga Kisangani ''B'' jirani na Saigoni amemuua mpenzi wake kwa kumnyonga na kumtumpa katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' Chini ya Shule ya Msingi Kilimahewa.
Taarifa zinasema mara baada ya mwanaume kudhamiria kutekeleza tukio hilo lililo kinyume na neno la MUNGU katika kitabu kile cha Kutoka 20.13 alimwambia mpenzi wake kuwa; "Leo nimejisikia tutoke out twende Beach za Gorden tukajivinjari" Mwanamke (Mama Koku) bila shaka lolote aliongozana nae mpenzi wake huyo ndipo wakiwa njiani katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' mwanaume alimbadilikia ghafla na kumkaba kooni mwanamke na kupelekea kupoteza maisha.
Comments
Post a Comment