WEMA SEPETU:NAJUTA KUWA NA DIAMOND

Takribani  wiki  sasa  kumekuwa  na  taarifa  zinazoeleza  kuwa  Miss  Tanzania  2006, Wema  Sepetu  hayuko  sawa  katika  mahusiano  yake  ya  kimapenzi  na  nguli  wa  Bongo  Fleva, Diamond  Plutnumz….
Kwa  mujibu  wa  rafiki  wa  karibu  na  Wema, imefika  mahali  Wema  anajuta  kuwa  na  Diamond  kwa  sababu  ya  kuandikwa  kwa  mambo  mengi  yasiyo  na  ukweli  na  yanayomfedhehesha  moyoni….
Rafiki  huyo  amedai  kuwa  mara  kwa  mara  Wema  amekuwa  akijiuliza  sababu  ya  kuandikwa  taarifa  mbalimbali  zisizo  na  kichwa  wala  miguu  ambapo  mwisho  wa  yote  hupata  jibu  ni  kwa  sababu  ya  kuwa  na  mahusiano  na  Diamond….
“Wakati  mwingine  anasema  angelijua  bora  angebaki  bachela  kwani  kuna  kikundi  cha  watu  hakipendi  kumuona  akiwa  na  Diamond  hivyo  kinafanya kazi  ya  kumzushia  taarifa   zisizoeleweka  kila  mara  kwa  lengo  la  kumshushia  hadhi,” kimesema  chanzo  hicho.
 
Mwandishi  alipokiuliza  chanzo  hicho  ni  kwa  kiasi  gani  Wema   anamwamini  Diamond  kilisema:
“Ukweli  ni  kwamba  Wema  anampenda  sana  Diamond  lakini  hamwamini  kwa  sababu  wakati  mwingine  taarifa  zinazoandikwa  magazeti  hutolewa  na  Diamond  mwenyewe, hali  hiyo   inampa  wakati  mgumu  sana  Wema  kujua  ashike  wapi  na  wapi  apaache,” 
wemadiamond 
“Unajua  Diamond  haaminiki, unaweza  kukuta  Wema  anagombana  na  watu  kumbe  mtoa  taarifa  ni  Diamond  mwenyewe.”

Comments