Sony Music Africa pamoja na Rock star 4000 wametangaza list ya mastaa watatu kutoka Afrika Mashariki ambao watashiriki kwenye stage moja ya show kubwa itakayowashusha mastaa wa dunia nchini Afrika Kusini.
Mastaa wa Uganda waliotangazwa ni Maurice Kirya aliewahi kufanya kolabo na Ay, Keko pamoja na Naava ambao watashiriki kwenye stage moja na Nicki Minaj, J Cole, Ryan Lewis, Macklemore, Kid Ink na wengine wengi.
Mastaa wengine wa Afrika waliochaguliwa ni D’Banj na Tiwa Savage kutoka Nigeria, Liquideep wa South Africa ikiwa ni tamasha ambalo litashirikisha Wasanii zaidi ya 300 kutoka sehemu mbalimbali duniani pamoja na MaDj mia moja kwenye zaidi ya majukwaa 60 kuanzia September 26 – 28 ambapo Naava atamiliki stage September 26, Maurice Kirya Sept27 na Keko Sept. 28.
Unaambiwa ni tamasha la kila mwaka ambapo time hii litawakutanisha mashabiki zaidi ya laki moja kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Comments
Post a Comment