TLC WAIKANA INTERVIEW WALIYOMPONDA RIHANNA

TLC 
Kama unakumbuka wiki iliyopita moto uliwaka kwenye mitandao ya kijamii hasa twitter baada ya waimbaji wa kundi la TLC, T-Boz na Chilli kuonekana kwenye kituo cha runinga wakitoa maoni yao yanayoonekana yanamchana Rihanna kwa kuvaa nusu uchi kwenye tuzo za CFDA.

TLC AYAA 
Baada ya interiview hiyo kuruka ni kama walitangaza vita na Rihanna na yeye akajibu kwa kuwachana kwenye twitter na kisha kupost picha inayowaonesha waimbaji hao wakiwa kifua wazi enzi zao huku wameficha ch*chu.
Waimbaji hao wamefanya mahojiano na Yahoo! Music na kuikana interview waliyofanya kwa madai kuwa ilifanyiwa uhariri na kuungwaungwa na kisha kuwekewa picha za Rihanna wakati wanatoa maoni ya kuwashauri wasichana wadogo kuhusu namna ya kujitunza.
Walisema hata wao walipoiona interview hiyo walishangaa kwa kuwa hawakumaanisha kile kilichooneshwa na kwamba kwa ushahidi zaidi hakuna sehemu ambayo walitaja jina la msanii yoyote na kwmba walikuwa wanaongelea vipindi vya runinga.
T-Boyz aliongeza kuwa kuna mtu alimuuliza kama ameshamuona Rihanna na yeye akamwambia bado kwa siku za hivi karibuni kwa kuwa walikuwa Australia na hata hawakumuona Rihanna kwenye tuzo za CFDA kwa kuwa walikuwa busy na mambo yao Australia na hawakujua kama kuna tuzo zinatolewa.
Kuhusu picha iliyowekwa na Rihanna wakionesha vifua vyao, “Ile picha nilipiga nikiwa na miaka 22 na ilikuwa kwa ajili ya kuwafahamisha zaidi watu kuhusu saratani ya matiti.”
Wanadai kama wakionekana katika hali hiyo kwao ujue kuna sababu muhimu ya kufanya hivyo.

Comments