TAARIFA MPYA YA WAZIRI KUHUSU UGONJWA WA EBOLA NI HII HAPA


Ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umeingia kwenye headlines za dunia kutokana na kuripotiwa kwenye nchi mbalimbali za Afrika sasa umeingia kugusa vichwa vya habari na kuihusisha Tanzania. Waziri wa Afya wa Seif Rashid amesema wagonjwa waliohisiwa kupata maambukizo hayo kutokana na dalili za awali ni kutoka Benin na Mtanzania lakini baada ya vipimo wameonekana hawana maambukizo hayo.Waziri Seif Rashid amesema kuwa tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo ikiwa ni kauli iliyotoka baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliohisiwa.

 Kupitia ukurasa wake wa facebook, Waziri Seif amesema vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa vimewekwa pia huku wizara ya afya ikiongeza uwezo wa kufanya uchunguzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia.

Comments