SPIDER WOMAN KUTOKA MWAKA 2017

Spider woman 
Kama umekuwa ukifuatilia filamu za Spider-Man basi hii itakuwa stori nyingine itakayokufanya uzidi kuzipenda filamu hizi. Hivi karibuni Studio za Sony Pictures na mwongozaji wa filamu za Spider Man Marc Webb wamethibitisha kuwa na wazo la kuongeza mwigizaji wa kike kwenye filamu zao za mashuja na kama alivyokuwa Spider Man sasa huyu  ataitwa Spider Woman.

Kilichofahamika mpaka sasa ni kuwa wazo hilo lipo na linafanyiwa kazi,filamu itakayokuwa na Spider Woman itatoka mwaka 2017 sababu ya kuchelewa kwa kutoka kwa The Amazing Spider-Man 3 ambayo imetajwa kutoka 2018.

Comments